Tulio wengi tunapenda kutumia ukwaju japo wachache sana hawapendelei wakidai kwamba unakwangua utumbo na kuweza kuababisha vidonda vya tumbo
,lkn hapana ukwaju unafaida sana kwa afya zetu ,mimi binafsi na upenda sana japo nakumbuka kipindi cha miaka hiyo bado niko mdogo unapita kigengeni unanunua unaweka chumvi unakula co hivyo tuu ,bali unaweza kutengeneza juice ukanywa.
ukwaju(tamarind) |
UANDAAJI WA JUICE YA UKWAJU
Juice ya Ukwaju |
- andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu
- baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni
- uache uchemke hasa ht kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu
- ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe
- andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
- weka sukari kwa kiasi unachopendelea
- pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste
- weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa
Faida 10 za ukwaju:
- Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
- Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
- Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
- Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
- Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
- Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
- Husaidia kurahisisha choo (laxative)
- Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
- Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
- Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)
NB: Ikiwa ukwaju na asali havikudhuru, basi changanya hivyo viwili ili kupata faida maradufu!