Wednesday, August 15, 2012
Tuesday, July 31, 2012
MAPISHI YA VIBIBI
MAHITAJI
1.Mchele Vikombe 2
2. Tui la nazi Kikombe 1 na nusu
3. Mafuta kijiko 1 cha chakula
4. Hamira Vijiko vya chai 2
5. Unga wa ngano kijiko 1 cha chakula
6. Hiliki kiasi upendavyo
7. Sukari Kikombe 1
JINSI YA KUANDAA
1· Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
2· Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
3· Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
4· Ukishafura , mimina sukari na changanya vizuri ; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
5· Weka chuma kipate moto.
6· Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
7· Utazame ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
8· Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote,panga kwenye sahani na tayari kuliwa.
VIBIBI KATIKA PICHA. |
ENJOY YOUR MEAL
PISHI LA KATLES
MAHITAJI
1. Viazi Ulaya Nusu Kilo
2. Kitunguu swaum Kikubwa 1
3. Myama ya kusaga Robo
4.Limao
5.Vitunguu Maji Vikubwa 3
6. PiliPili Manga
7. PiliPili mbuzi
8. Mayai 2
9. Mafuta kiasi
10. chumvi.
11.unga wa ngano kikombe 1
JINSI YA KUANDAA
menya viazi vyako na uvioshe vizuri kwa maji safi
weka kwenye sufuria na uweke chumvi kiasi
weka jikoni vichemke hadi viwe laini .
wakati viazi viko jikoni andaa nyama yako ya kusaga
weka chumvi,ndimu,swaum,tangawizi,na pilipili manga,na km utapenda kuweka pilipili mbuzi
katiakatia vitunguu maji na uweke jikoni nyama nayo iwive.
viazi vikiwa tayari mwaga maji na uhakikishe hamna maji na uanze kuviponda hadi madonge yaishe.
nyama ikiwa tayari epua na uweke pembeni ipoe.
weka ndimu ktk viazi vilivyopondwa pamoja na pilipili manga kiasi changanya kwa pamoja.
tengeneza shape ya duara ukiweka kishimo kati kwa ajili ya kuweka nyama ya kusaga.
tengeneza madonge yako huku ukiweka nyama kati na kufunga kwa kutumia viazi vilivyopondwa.
baada ya kumaliza madonge yote .
andaa mayai kwenye kibakuli na uyachanganye alafu weka chumvi.
weka mafuta jikoni yachemke
then chukua donge moja moja zamisha kwa unga wa ngano (husaidia kutokuvurugika) halafu dumbukiza kwa mchanganyiko wako wa mayai na uweke kwenye mafuta.
kaanga hadi vibadilike rangi ,
katlesi zako ziko tayari kwa kuliwa..
na katlesi zako zitakuwa hivi katika picha.
ENJOY YOUR MEAL.
Saturday, March 10, 2012
TIA GET TOGETHER PARTY MSASANI BEACH CLUB
Tulifurahi sana cku hii with collage mates ,kula ,kunywa,kucheza,na kila kitu was there
Monday, February 27, 2012
BFF JAMANI SINCE ZANAKI ,,,,
this sunday nlikuwa na mafriends jamani tumetoka mbali since enzi za mama Mramba duuh hadi ss ,,
best friends for ever
naisubiria hiyo get tugether lols niwaone wote warembo wa mramba ,,,uuwii cant wait dears ..
zaituni malonji unatutamaniaje huko marekani unatamani ufly ..mis yu my habibty
best friends for ever
from left: witty,rose,nuru,and zahra |
rose,nuru witty,kithuraah |
me n zahra |
me n nuru |
nlilipenda hili pozi |
only me Wa kaumo |
zanaki girls ,,mwaah |
me n witty |
zaituni malonji unatutamaniaje huko marekani unatamani ufly ..mis yu my habibty
Friday, February 10, 2012
CHAGUA MSHONO UTAOKUVUTIA KULINGANA NA SHEPU YAKO
Monday, January 16, 2012
JUA JINSI YA KUTENGENEZA JUICE YA UKWAJU NA FAIDA ZAKE KTK MWILI
Tulio wengi tunapenda kutumia ukwaju japo wachache sana hawapendelei wakidai kwamba unakwangua utumbo na kuweza kuababisha vidonda vya tumbo
,lkn hapana ukwaju unafaida sana kwa afya zetu ,mimi binafsi na upenda sana japo nakumbuka kipindi cha miaka hiyo bado niko mdogo unapita kigengeni unanunua unaweka chumvi unakula co hivyo tuu ,bali unaweza kutengeneza juice ukanywa.
ukwaju(tamarind) |
UANDAAJI WA JUICE YA UKWAJU
Juice ya Ukwaju |
- andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu
- baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni
- uache uchemke hasa ht kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu
- ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe
- andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
- weka sukari kwa kiasi unachopendelea
- pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste
- weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa
Faida 10 za ukwaju:
- Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
- Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
- Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
- Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
- Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
- Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
- Husaidia kurahisisha choo (laxative)
- Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
- Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
- Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)
NB: Ikiwa ukwaju na asali havikudhuru, basi changanya hivyo viwili ili kupata faida maradufu!
Subscribe to:
Posts (Atom)